ISHA MASHAUZI AKIRI KUTUMIA MIRUNGI...!!



STAA wa muziki wa taarab na mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Aisha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’ ameibua gumzo na kushangaza mashabiki baada ya kukiri kuwa yeye ni mtumiaji wa pombe kali na madawa ya kulevya aina ya mirungi, Ijumaa Wikienda linashuka nayo.

Ishu hiyo ilijiri Alhamisi ya wiki iliyopita wakati akihojiwa na mtangazaji wa Redio Times FM, Hadija Shaibu ‘Dida’ kupitia kipindi chake cha Mitikisiko ya Pwani ambapo alisema mirungi na pombe kali ndiyo starehe yake kwani inampa stimu kabla hajapanda jukwaani na katika maisha yake ya kawaida nje ya usanii.
Mashauzi alifunguka hayo baada ya Dida kumtaka atoe ufafanuzi juu ya skendo ya kuvuta bangi inayomkabili ambapo alisema siyo kweli kwamba anavuta bangi ila akakiri kuwa anakula sana mirungi na kugida ulabu. Aliongeza kwamba kwa kuwa hana mume, mtoto wala hataki kuwa na familia, mirungi na pombe ndiyo vitu vinavyompa furaha maishani mwake.
Ijumaa Wikienda lilipomtafuta Mashauzi ili kuipata ishu hiyo kiundani, alijibu kuwa hayo ni maisha yake hivyo kama anatumia mihadarati asifuatwefuatwe kwani ndiyo aina ya maisha aliyoyachagua.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter