HUKUMU YA KAJALA NA MUMEWE KUSOMWA LEO(JUMATATU).....!!



HUKUMU ya kesi inayomkabili staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja inayotarajiwa kutolewa leo (Jumatatu) na Hakimu Sundi Fimbo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar itakuwa ya kishindo na mastaa wengi presha zimekuwa zikipanda na kushuka.

Kajala anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe, Faraji Agustino kukumbwa na msala wa kutakatisha fedha haramu.
Wakizungumza na Ijumaa Wikienda juzikati, baadhi ya mastaa ambao muda mwingi wamekuwa wakiutumia kumuombea msanii huyo walisema kuwa wanajua hukumu hiyo itakuwa ya kishindo ila wao wamechukua nafasi yao kwa maombi na sasa wamemuachia Mungu.
“Wengi tumekuwa tukishindwa kula wala kufanya mambo yetu kutokana na hili linalomkabili mwenzetu ila leo (Jumatatu) mbivu na mbichi zitajulikana,” alisema Julieth Isack, msanii chipukizi aliyedai kuwa mmoja wa watu wa karibu wa Kajala na kuongeza:
“Kila mmoja amekuwa na shauku ya kujua hukumu hiyo itakuwaje ila tunaamini haki itatendeka na mambo yatakwenda vizuri.”

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter