Sehemu ya ng"ombe wanaopelekwa kwa ajili ya mahali
Zahanati ya kijiji cha Malangali ambayo mwanafunzi huyo alikuwa akipima na sasa ameamua kuikwepa zahanati hiyo kukwepa mkono wa sheria
** Kufuatia sakata hilo Diwani viti maalumu atishiwa kuuwawa
** Polisi waingilia kati sakata hilo
Mkazi wa Kijiji cha Mpona Kata ya Totowe Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya anatuhumiwa kumwachisha masomo mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Totowe kwa kumuoa kisha kumpa ujauzito.
Mwananchi huyo aliyefahamika kwa jina la Ndugu Shigala Mwachanya anatuhumiwa kutenda kosa hilo kwa kumpa ujauzito mwanafunzi aliyejulikana kwa jina la Ngolo Jiguma(19) ambaye amesitisha masomo yake kutokana na ujauzito alionayo ambapo wazazi walipatana kulipana Ng’ombe 45 kama fidia ambapo tayari Ng’ombe 20 wameshatolewa.
Aidha kutokana na Mwanafunzi huyo kutambua kuwa Wazazi wake wametenda kosa ameamriwa kuto hudhulia kliniki katika kituo cha afya cha Malangali na badala yake amekuwa akienda katika Zahanati ya Totowe ili kukwepa kukutwa na vyombo vya sheria.
Uongozi wa Kijiji hicho umeanza kulifuatilia sakata hilo baada ya kupata taarifa kutoka kwa Mkuu wa Shule aliyokuwa akisomaMwanafunzi huyo Frank Mwakisyala ambapo juhudi hizo zinaonekana kugonga ukuta kutokana na kutishiwa kuawa na mtuhumiwa.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho Ndugu Yaledi Mwanguku amesema kuwa suala hilo lipo juu ya uwezo wake hivyo alilazimika kulipeleka suala hilo kwenye uongozi wa kata kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Diwani wa Viti Maalumu kata hiyo Christina Kibwana ambaye alionekana kulipokea suala hilo na kuanza kulifuatilia pia alidai kuwa alipokea ujumbe mfupi wa maandishi ukimtaka ahame kijijini hapo lasivyo aache kulifuatilia sakata hilo na asipoacha angeuawa.
Diwani huyo amesema ujumbe huo wenye maneno ya kutishia yalikutwa kwenye barua nje kidogo nje ya nyumba yake ambapo aliongeza kuwa baada ya kuona hali hiyo aliamua kutoa taarifa katika kituo kidogo cha Polisi cha Galula Wilayani Chunya.
Diwani huyo ameendelea kulalamika kuwa baada ya kutoa taarifa katika kituo hicho hakuna dalili wala hatua zozote zilizochukuliwa ambapo alisema kuna dalili za Rushwa ambayo inasemekana kuwa Polisi walipewa Rushwa ya Shilingi Milioni Moja na Nusu(1500,000/=).
Amesema kutokana na kutoonekana kwa hatua zozote aliamua kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Chunya ambapo walimkamata mtuhumiwa huyo kisha kufunguliwa kesi katika Mahakama ya Wilaya ya Chunya.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Totowe kupitia Chama cha Mapinduzi, Godian Wangala amethibitisha kutokea kwa matukio yote hayo na kuongeza kuwa amesikitishwa na kitendo cha Mwananchi huyo pamoja na wazazi kwa kumwachisha masomo na kumsababishia Mwanafunzi kumnyima haki ya kupata elimu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amekiri kupokea taarifa hizo na kuahidi kulifanyia kazi kwa ukaribu zaidi na kuhakikisha wahusika watachukuliwa hatua zinazostahili.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....