Prodyuza huyo mkubwa wa filamu za Kibongo alisema kuwa ilifika ‘taimu’ akawa anapiga kelele ovyo ndani ya nyumba yao kutokana na kubanwa na mawazo.
Alifunguka kuwa kila mumewe alipomuona na hali hiyo alikuwa akimuomba atulie na kumwambia akiendelea atakuwa chizi.
“Sajuki alikuwa akiniambia ananionea huruma sana kutokana na hali niliyokuwa nayo.
“Yaani nilijua naaga dunia kiukweli kwani nilikuwa nawatumia watu meseji kuwaomba msamaha kama nimewakosea kwa sababu kila nilichofanya kilikuwa hakiendi,” alisema Wastara.
Wastara alisema kuwa aliichukia wodi aliyolazwa mumewe katika Hospitali ya Muhimbili, Dar kwani ndani ya wodi hiyohiyo aliwahi kulazwa mama yake mzazi ambaye naye alifia wodini hapo miaka ya nyuma.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....