MSANII aliyewahi kufanya vizuri kwenye game la muziki miaka kadhaa nyuma Q-Chillah, ameamua kufungua na kueleza sababu iliyomfanya kuanza kutumia dawa za kulevya, huku akidai kuwa ugumu wa maisha ulichangia kwa kiasi kubwa kwani watu wake wa karibu walimkimbia na kumuacha hakiwa hana wa kumuongoza.
Q-Chillah alitoa maneno wakati akizungumzia kwenye moja ya vipindi vya radio, ambapo alisema kuwa hakuwaza kama angetumia dawa hizo lakini ilitokea baadhi ya watu wake wa karibu kumtosa kwenye kila ishu.
Alisema kuwa aliamua kutumia dawa hizo ili kumtoa kwenye usongo wa mawazo aliyokuwanayo lakini hakujua kama anaongeza mawazo na matatizo kwani alipokuwa akitumia alijihisi mtu mwenye furaha lakini kumbe ni ishu ya hatari aliyokuwa akifanya.
Chillah alisema kuwa ugumu wake wa maisha ulikuja baaada ya muziki wake kuwa hauna soko kwani alikuwa akifanya vizuri lakini bado ulikua haupokeliwi kwa mikono miwili na mashabiki wake.
Alisema kuwa pia kuna baadhi ya watu walikuwa wakimfanyia fitna kwani alipokuwa akitoa kazi wakilitumia kila mbinu ili kazi zake zisitoke na watu kuzijua, huku wakijua wazi kuwa wanamkosesha hela na hali hiyo ilikfanya kujiona mpweke, ingawa hajui nani aliyemkosea.
“Soko langu la muziki liliyumba sana kwani nilikuwa nafanya kazi nzuri lakini bado sokoni zilikuwa hazifanyi vizuri, pia kuna baadhi ya watu walikuwa wanafitna juu yangu kwani kazi nyingi nilizokuwa natoa walizikalia ili mashabiki wake wasizipate,” alisema Q-Chillah.
Hata hivyo aliongeza kuwa anamshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kumsaidia msanii mwenzake Ray C, ambaye naye alikuwa kwenye hali ngumu baada ya kuzidiwa na matumizi hayo ya adwa ya kulevya.
Pamoja na hayo msanii huyo aliwaomba wasanii wote wanaotumia dawa za kulevya kujitokeza hadharani ili wapewe msaada bila hivyo watajikuta kwenye matatizo makubwa, ambapo kwa upande wake alisema kuwa ameamua kuachana na dawa hizo kwa kumrudia mungu wake.

0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....