MAAJABU: MWANAMKE AJIFUNGUA KAMBA YA MANILA

MWANAMKE aliyefahamika kwa jina la Lea Lika, hivi karibuni ‘alijifungua’ kamba ya manila baada ya kusumbuliwa na ujazo wa tumbo kwa miaka 31.

Lea Lika akitoa ushuhuda kwa waumini wa Huduma ya Neno la Upatanisho (WRM) iliyopo Kivule, Dar, Jumapili iliyopita.
Akitoa ushuhuda uliowatoa machozi waumini wa Huduma ya Neno la Upatanisho (WRM) iliyopo Kivule, Dar, Jumapili iliyopita, Lea alisema kuwa kwa muda wote huo tumbo lake lilionekana ni mjamzito.
Lea alisema, siku ya tukio alijisikia kutaka kutoa kitu kikubwa akaenda chooni kwa lengo la kujisaidia ambapo alishangaa kuona anatoa kamba ya manila, hali iliyompa hofu na kutaka kukimbia.
 “Mume wangu alikuwa nyuma ya nyumba, nilimuita ili aje kunisaidia. Alipofika alichukua kitambaa na kushika manila kisha kuanza kuivuta, ilitoka ndefu sana tena ikiwa imefungwa vifundo viwili. Ni ajabu sana,” alisema mwanamke huyo.
 Alisema siku alipofika kwenye Huduma ya WRM, Nabii Nicolaus Suguye alimwambia ametupiwa majini.
“Kwa kipindi cha miaka 31 nilikuwa siwezi kufanya kazi yoyote kutokana na maumivu makali mwilini mwangu,” alisema Lea.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter