‘H-BABA’ KUWAFUNDA WANAUME WANAOPENDA KUTEMBEA NA WANAWAKE BILA MALENGO NDANI YA NGOMA YAKE YA ‘FUNGA ZIPU’…!!

http://dartalk.com/wp-content/uploads/2013/01/h_baba.jpg

BAADA ya kufanya pouwa ndani ya mwaka jana, msanii H-Baba, amesema kuwa anatarajia kufungua mwaka huu na ngoma mpya inachowahusu wanaume wanaopenda kutembea na wanawake bila malengo aliyoipa jina la ‘Funga Zipu’, ambayo hivi karibuni itakuwa hewani ambapo itakuwa sambamba na video. 
Alisema kuwa kwa sasa anafanya utaratibu wa kutengeneza DVD ambazo zitakuwa zinaonesha show zake zote alizopiga mwaka jana pamoja na zile alizopiga na JB Mpiana msanii mahiri kutoka Congo, ambayo itakuwa sokoni mapema Februari mwaka huu.
H-Baba aliongeza kuwa kutokana na tabia chafu walizonazo wasanii za kuibiana kazi sasa anafanya utaratibu mpya kwa yeyote atakahusika na wizi wa kazi zake atamchukulia hatua kali ikiwemo kumpeleka mahakani ili iwe fundisho kwa wengine ambao wanashindwa kutumia akili zao badala yake wanasubiri kuiba kazi ya mtu.
“Natarajia kufungua mwaka na kazi nyingi lakini ngoma yangu ya ‘Funga Zipu’ ndiyo itakayoanza hivyo nawaomba mashabiki wangu ambao nipo nao miaka yote kuisubiri kazi hiyo kwani ni hatari na hawa wanaopenda kuiba kazi zangu watasubiri,” alisema.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter