Katika hali isiyo kuwa ya kawaida diwani mmoja wa chama cha siasa jina laka na chama chake limewekwa kapuni kwa sasa amefumaniwa akivunja amri ya sita na mke wa mtu usiku wa leo na kuchezea kichapo .
Diwani huyo mpenda ngono anadaiwa kufumaniwa akiwa katika nyumba ya mpiga kura wake huyo katika kata kata moja ya wilaya ya Iringa Vijijini na ni diwani anayetokea katika wilaya ya Iringa mkoa wa Iringa na ni diwani mtanashati kweli kweli.
Mashuhuda wa tukio hilo wameudokeza mtandao huu wetu kuwa kutokana na fumanizi hilo la mwaka wapiga kura wake wanaoishi jirani na nyumba hiyo ambayo mheshimiwa alifunaniwa waliizunguka nyumba hiyo na kuanza kumshikisha adabu mheshimiwa huyo.
Baada ya mheshimiwa huyo kuchezea kipigo kutoka kwa njema lenye mke huyo pamoja na wananchi alilazimika kutoka mbio na kukimbilia porini kabla ya kwenda kupatiwa matibabu katika moja kati ya zahanati mbili zilizopo katika eneo hilo ikiwemo ya Misheni na ile ya Kijiji .
Iwapo wataka kujua zaidi juu ya tukio hili endelea kufuatilia mtandao huu unapofanya jitihada za kumtafuta diwani huyo
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....