Siku chache baada ya kufariki mwigizaji Sajuki, rafiki yake wa siku nyingi mwigizaji Dinno ameongea na AMPLIFAYA ya CLOUDS FM na kutaja moja kati ya mipango mikubwa aliyokua nayo Sajuki.
Namkariri akisema “kuna watu wako Denmark tuliwasiliana nao walisema tusajili kampuni ambayo inajulikana kiserikali, Sajuki akasema sababu mimi naumwa we fanya huo mchakato mwambie Wastara uwe unakwenda nae, hao jamaa walitaka kufanya kazi na sisi”
“Pia wakati kipindi kile anatibiwa India kwenye hospitali ya mastaa wa movie walisikia kwamba kuna mwigizaji kalazwa pale ambae ndio Sajuki kwa hiyo baadhi ya waigizaji wa India wawili watatu walikuja kumtembelea wakamweleza, safari hii aliniambia akirudi India alitaka akae hata miezi mitatu ili awacheki wale jamaa wajue mpango wa kufanya kazi” – Dinno
Unaweza kumsikiliza Dinno hapa chini pia.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....