Kufuatia kugubikwa na skendo lukuki zikiwemo ushoga, umalaya, ukuwadi, usagaji na uchafu wa kila aina ndani ya tasnia ya filamu za Kibongo (Bongo Movies), staa ‘legendary’ wa kiwanda hicho, Salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ ameanika kuwa mambo hayo ndiyo yanayowaharibia kazi zao kwenye jamii.
Thea mwenye takribani miaka 10 ndani ya sanaa hiyo aliiambia Funguka na kusema kuwa kwa sasa tasnia ya filamu za Kibongo imechafuka kwa skendo tofauti na ilivyokuwa zamani.
Alisema kuwa yanayofanyika ni aibu hata kwa wasanii kujiita kioo cha jamii hivyo kuomba asionekane mbaya kwa kusema ukweli kwa nia njema tu .
Mwandishi : Unafikiri ni nini sababu ya tasnia ya filamu kugeuka kichaka cha kufanyia uovu tofauti na ilivyokuwa zamani?
Thea: Sababu kubwa ni wasanii wanaoingia kwenye tasnia bila kujua maadili ya uigizaji na utaratibu wake kwani ukiangalia wanaofanya uchafu huo hawajapitia kwenye vikundi vya sanaa na hawajui maana ya uigizaji.
Mwandishi Mbali na wasanii ambao hawajapita kwenye vikundi, wapo pia waliopitia huko (kwenye vikundi vya sanaa) lakini nao wanatajwa kwenye skendo za usagaji na ushoga. Hili unalionaje?
Mwandishi Ni kweli wapo baadhi wanaofanya hivyo na ukweli ni kwamba hawa kaka zetu wanatutia aibu sana na kinachowaponza ni tamaa za kutaka mafanikio ya haraka. Hawajui kuwa Mungu amempangia kila mtu riziki yake, matokeo yake wanafanya uchafu ili waonekane wana magari ya kifahari.
Mwandishi: Unalizungumziaje suala la ushirikina kwenye tasnia ya filamu kwani waigizaji wengi wamekuwa wakilalamika kuwa wanalogwa na wengine wakionekana wanakuja juu kwa kasi hivyo kuhusishwa na ulozi?
Mwandishi: Nimesikia habari hizo lakini mimi siamini uchawi na hakuna anayeweza kuniloga kwa sababu nina Yesu ambaye hakuna linaloshindikana kwake.
Mwandishi : Je, unazungumziaje hili la waigizaji ambao wanatajwa kujihusisha na ushirikina na wanakuja juu kwa kasi?
Thea: Jamani wasanii wenzangu kama mnafanya hivyo acheni na tukubali mabadiliko kwenye sanaa kwani kila siku vinazaliwa vizazi vipya kwa hiyo kila mtu ana wakati wake wa kupanda.
Mwandishi Vipi kuhusu skendo ya umalaya iliyoshamiri kwa wasanii wa kike ndani ya tasnia ya filamu?
Thea: Ni kweli wasanii wa filamu ni malaya sana na asilimia 90 ya waigizaji wa kike wapya ndiyo wanaoongoza kwa kuchafua tasnia kwani kila uchafu uko ndani ya filamu. Mara kukaa utupu, ukuwadi, kugombea mabwana na mengine mengi yasiyopendeza mbele ya jamii.
Mwandishi Ni kitu gani kifanyike ili kuondokana na uchafu wote huo?
Thea: Nawashauri wamuombe Mungu sana na waachane na maisha ya kuiga na kutamani vitu ambavyo hawawezi kuvipata. Wasanii wafanye kazi kwa bidii ili waweze kufikia malengo yao.
Mwandishi: Tofauti na skendo ulizozungumzia, pia kuna suala la wasanii kujitenga makundi-makundi, hili likoje?
Thea: Sitaki kulisemea sana hilo kwa sababu Tanzania ilipiganiwa na watu wachache mpaka tukapata uhuru hivyo tasnia ya filamu nayo itapiganiwa na wasanii wachache na taratibu tutafika kwenye usemi na lugha moja.
Mwandishi:
Baada ya kuwaona wasanii wakifanya mambo machafu huwa unawasaidiaje ukiwa kama mwigizaji mkongwe?
Thea: Sina cha kuwasaidia kwa sababu katika kuingia kwenye filamu kuna watu waliwashika mkono na kuwasaidia hivyo haohao wanatakiwa kuwasaidia kimawazo na ushauri ili wabadilike lakini wao ndiyo wanawafanya mabibi na mabwana zao, mimi wale niliowasaidia lazima niwafundishe maadili ya uigizaji.
Mwandishi: Hivi sasa wakongwe mmekuwa kimya sana na mnaonekana kupitwa na wasanii wapya wanaoingia kwenye filamu, kwako hili unalionaje?
Thea: Unajua pumba na mazao huwa vinajitenga, wapo wasanii wanaoingia na kuwika sana lakini hawadumu, wanapotea kwa muda mfupi.
Mwandishi: Je, umejipanga vipi kukabiliana na changamoto za wasanii chipukizi?
Thea: Kila kazi ina changamoto zake kwa sababu zamani tulibweteka kwani tulikuwa wachache ila mpaka sasa sijaona mtu wa kunitisha kwa wanaokuja.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....