“NILIWAHI KUSHAURIWA NIENDE KWA MGANGA KUCHUKUA DAWA ZA KUNIWEKA JUU KWENYE MUZIKI” – KALA JEREMIAH…!!


MSANII wa muziki wa Hip Hop anayetamba na ngoma yake mpya ya ‘Dear God’, Kala Jeremiah, amesema kuwa wapo baadhi ya rafiki zake na watu wa karibu waliwahi kumshauri aende kwa mganga kwa lengo la kuchukua dawa ili aongeze nguvu kwenye muziki wake.

Msanii huyo amefunguka juu ya ishu hiyo baada ya track yake hiyo mpya, kwenye moja mistari yake anaeleza kuwa aliwahi kushauriwa aendekwa mganga, ndipo mwandishi
huu alipomtafuta ili aweze kufafanua juu ya ishu hiyo, Kala alisema kuwa hayo ni maneno ya kweli kwani kuna baadhi ya watu waliwahi kumshauri aende kuchukua dawa kwa mganga ili muziki wake ushike kasi.

Alisema kuwa baada ya kuambiwa maneno hayo alishindwa kuelewa ni kwa nini lakini alikuja kujua kuwa kuna baadhi ya wasanii ambao wanatumia dawa za kishirikina kwa imani kuwa waweze kufanya vizuri katika kila ngoma wanayotoa.


Alisema kuwa kwa upande wake aliachana na habari hizo kwani anaamini kiwango chake ni kikubwa sana na haoni sababu ya yeye kujihusisha na ushirikina.


“Ni kweli kuna baadhi ya watu waliwahi kuniambia niende kwa mganga ili kuongeza nguvu katika muzki wangu, lakini kamwe huwezi amini kwamba sina muda na uchafu wa namna hiyo na hata kama ngoma zangu zikiwa hazifanyi vizuri kwenye gemu haina noma kwa sababu naamini katika kipaji changu,alisema.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter