Vuta nikuvute hiyo imetokea eneo ambalo ni nje ya jiji kidogo ambapo binti mmoja alipokamatwa na Wanachi wenye hasira kali kwa shutuma za wizi.
Tukio hilo ambalo lilitokea majira ya mchana Lilizua jambo zito pale binti huyo alipokamatwa akiiba Nguo ambazo zilikuwa zimeanikwa kwenye kamba kama ilivyokuwa kawaida ya wananchi wengi hapa Nchini.
Reporter anazidi kutupasha kuwa kabla ya tukio mwanadada huyo alionekana mara kwa mara maeneo hayo huku wengi wao kutoelewa ujio wake mtaani hapo kwa wakati ule, "Mi nilishangaa kwasababu sikuwahi kumuona huyu dada hapa mtaani kwetu hata siku moja, Ila mara ya kwanza nilijua ni mgeni wa mwenyeji mmoja ambaye yupo mtaani kwetu hapa" Alisema dada mmoja mbaye alikuwepo eneo la tukio.
Mtaa huo ulipigwa na butwaa kubwa pale walipoona Ghafla kelele za mwizi , na mara tu walipotaka kutoka nje kuona ni nani huyo ambaye anaitiwa MWIZI ndipo walipokutana na dada yule ambaye alikuwa akizagaa mtaani hapo,
Kitu cha kushangaza katika mkasa huo ni kwamba wananchi waliohusika kumwadhibu mwanadada huyo walikuwa ni wanawake ambao walionesha kukerwa na kuaibishwa na tabia ya mwanadada huyo, hivyo hakuna mwanaume yoyote ambaye aliruhusiwa kunyoosha mkono kumpiga mwanadada huyo kwani walidai ati wao wanatosha kumwadhibu mwalifu huyo.
Tabia ya halifu kwa jinsia ya kike inaonekana kutapakaa zaaidi hapa nchini na wadadisi wa mambo wamegundua kuwa tabia hiyo inatokana na kichocheo kikubwa cha ugumu wa maisha na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwakabili wanawake hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....