WEMA, DIAMOND: MPAKA KIFO


MASTAA Abdul Juma ‘Diamond’ na Wema Sepetu wameonekana uhusiano wao utatenganishwa na kifo tu baada ya kunaswa pamoja tena wakisherehekea Sikukuu ya Eid Al-Hajj.

Mnyange Wema Sepetu akigonga menyu ya Eid nyumbani kwa akina Diamond Tandale jini Dar.
Habari kutoka kwa chanzo chetu makini, kwa sharti la kutochorwa jina lake gazetini, zinasema kwamba, wawili hao bado wanaendelea na uhusiano wao lakini wameamua kufanya siri ili wambeya wasiwafitini.
“Nilishasema Wema na Diamond hawawezi kuachana, watu wakabisha...ona sasa wapo pamoja, tena na mama mkwe (mama Diamond) wanakula Eid Tandale,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupata nyepesi hizo, gazeti hili lilianza upekuzi ambapo lilifanikiwa kunasa picha zilizozagaa mitandaoni zikiwaonesha Wema, Diamond na mama yake wakipata ‘rizki’ pande za Tandale katika nyumba iliyodaiwa kuwa walikuwa wakiishi zamani pande hizo.
Ili kupata ukweli wa habari hii, gazeti hili liliwasiliana na Diamond na kumwuliza kuhusu tukio hilo ambapo alisema: “Tandale ndiyo kwetu na siku zote katika maisha yangu siwezi kupadharau eti kisa nimekuwa maarufu.
“Waswahili wanasema, mdharau kwao ni mtumwa na mimi sitaki kuwa mtumwa ndiyo maana nikaamua Eid hii nile nyumbani kwetu. Nilishinda siku nzima nikibadilishana mawazo na watu wa kitaani kwangu maana hao ndiyo wamenilea.”
Alipoulizwa kuhusu uwepo wa Wema alisema: “Wema ni rafiki yangu, ni mtu wangu wa karibu. Mambo ya mapenzi tulishayaacha, kwa sasa namhesabia kama rafiki tu, kwa hiyo niliongozana naye kwa ajili ya kampani hakuna cha zaidi.”
Wema hakupatikana kuzungumzia tukio hilo baada ya simu yake kutopatikana muda wote ilipopigwa.

Diamond Platinumz (wa pili kulia) nae akipata msosi wa Eid nyumbani kwao Tandale.
Mama mzazi wa Diamond nae alikuwepo kusherehekea sikukuu hiyo ya Eid.
Wema akiomba kabla ya kupata msosi wa Eid.
Ndugu, jamaa na marafiki wa Diamond wakinawa kabla ya kupata msosi.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter