Shilole: Wasanii wa bongo hawaniwezi


Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na kundi lake wakiwa kazini.
Na Gladness Mallya
MWANADADA anayefanya vizuri kwenye tasnia ya Filamu na Muziki wa Mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amewaonya wasanii wa kike wanaotoka katika filamu na  kutaka kuingia kwenye muziki bila ya kujipanga.
Akichonga na Tollywood Newz, Shilole alisema kumekuwa na wimbi kubwa la wasanii wa kike wanaotoka katika filamu na kutaka kuingia kwenye muziki baada ya kumuona yeye anavyosumbua.
“Wengi wanataka kushindana na mimi lakini nawaambia kuwa hawataweza kufikia levo niliyonayo kwa kuwa nimejipanga kisawasawa,” alisema.
Mbali na hivyo, Shilole amewataka wasanii hao wa kike ambao wameshaanza kumtengenezea bifu kuwa hawatamuweza kwani  yeye ni mpiganaji asiyebweteka.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter