Rushwa ya ngono yanuka kwa wasanii wa bongo


Mainda.
Nisha.
Mwakifwamba.
Na Gladness Mallya
KIMENUKA,  kwa wasanii wapenda ngono kwani Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), chini ya Rais wake Simon Mwakifwamba limesema kuwa litawasaka wasanii wa kiume wapenda ngono.
 Hali hiyo imekuja kufuatia skendo ya baadhi ya waandaaji wa kiume kudaiwa kuwanyanyasa wasanii wa kike kwa kuwataka kimapenzi ili  kuwapa nafasi ya kuigiza.
Tino.
Akizungumza na Tollywood Newz, Mwakifwamba alisema anaandaa siku maalum kwa ajili ya kuzungumza na waandaaji hao baada ya kupata malalamiko kutoka kwa baadhi ya wasanii wa kike hivi karibuni Leaders Club, Kinondoni jijini Dar.
“Kama Rais wa Taff nimepokea malalamiko yao na ninayafanyia kazi,  nitazungumza nao maana hata mimi mwenyewe imeniuma na ninaona wasanii wa kike wanahitaji msaada zaidi,” alisema Mwakifwamba.
Baadhi ya wadau walisema kama Taff itachukua hatua hiyo, Bongo Movie hali itakuwa ni tete kwa wasanii hasa wa kiume.
Johari.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter