Picha Mbali Mbali zikionyesha Aunty Ezekieli Akiwa ndani ya Shela ya Arusi ya Kiislam ..Bi Dada ndio Kashaolewa hivyo ..Hongera zake sana Tunawatakiwa maisha mema yeye na Mume Wake ...Safiiiiiiiiiiiiii
KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akiwa chini ya ulinzi mkali, kujibu tuhuma tano zikiwamo wizi na uchochezi.
Tuhuma zingine ni kula njama, kuingia kwa nguvu kwenye eneo lisilo mali yake kwa nia ya kutenda kosa na kujimilikisha ardhi kwa nguvu na kusababisha uvunjifu wa amani.
Sheikh Ponda alifikishwa mahakamani hapo akiwa na watu wengine 49 akiwamo Bibi Zaina Yusufu (100), ambao waliunganishwa naye katika mashtaka manne isipokuwa shtaka la uchochezi ambalo linamkabili Ponda pekee.
Ponda ambaye anadaiwa kuwashawishi wafuasi wake kutenda makosa ya kihalifu alisomewa mashtaka, lakini alinyimwa dhamana baada ya Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka kuwasilisha mahakamani hati kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) inayozuia dhamana.
Hati hiyo ilitolewa chini ya kifungu cha 148 (4) cha sheria ya Mwenendo wa mashauri ya Jinai (CPA) na wakili Kweka aliomba iwekwe kwenye kumbukumbu za mahakama, hali iliyozua mabishano ya kisheria baina yake na wakili wa utetezi, Juma Nassoro .
Kufikishwa mahakamani
Ponda alifikishwa mahakamani hapo, jana saa 6:20 mchana na gari lililosindikizwa na magari mengine mawili aina ya Land Rover Defender; kila moja likiwa na askari zaidi ya watano wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) ambao walikuwa na silaha.
Pia msafara huo, uliongozana na gari la maji ya kuwasha pamoja na askari waliokuwa na mabomu ya kutoa machozi. Sheikh Ponda alipofikishwa mahakamani alitenganishwa na washtakiwa wengine na alikuwa amevalia kanzu huku miguuni akiwa hana viatu.
Alipelekwa moja kwa moja kwenye ukumbi wa Mahakama ya Wazi namba moja ambako aliwakuta washtakiwa wenzake 49. Washtakiwa hao wengine walifikishwa mahakamani hapo saa 5:15 asubuhi kwa karandinga.
Ilipofika saa 6:56 mchana, Hakimu Mkazi, Stuart Sanga aliingia mahakamani na kuanza kusikiliza kesi hiyo. Hata hivyo alieleza kuwa shauri hilo lilipangwa kusikilizwa na Hakimu Victoria Nongwa ambaye jana hakuwapo.
Baada ya kusema hivyo, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka alianza kuwasomea washtakiwa hao mashtaka yanayowakabili.
Mashtaka yao
Katika shtaka la kwanza, Wakili Kweka alidai kuwa Oktoba 12, mwaka huu katika eneo la Chang'ombe Malkazi, washtakiwa hao kwa pamoja walikula njama ya kutenda kosa kinyume na kifungu cha 384 cha sheria ya kanuni ya adhabu.
Katika shtaka la pili alidai kuwa Oktoba 12, mwaka huu, katika eneo hilo la Chang'ombe Malkazi lililopo wilaya ya Temeke, kwa jinai na pasipo sababu za msingi walivamia ardhi inayomilikiwa na kampuni ya Agritanza Ltd kwa nia ya kujimilikisha isivyo halali.
Wakili huyo alidai kuwa kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 85 na 35 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Katika shtaka la tatu, Kweka alidai kuwa kati ya Oktoba 21 na 16, mwaka huu katika eneo hilohilo, washtakiwa hao kwa pamoja pasipo uhalali wowote, walisababisha uvunjifu wa amani kwa kujimilikisha ardhi ambayo ni mali inayomilikiwa kihalali na Kampuni ya Agritanza Ltd.
Wakili Kweka katika shtaka la nne, alidai kuwa washtakiwa hao kwa pamoja kati ya Oktoba 12 na 16, waliiba vifaa na malighafi mbalimbali za ujenzi, yakiwamo matofali 1500, tani 36 za kokoto na nondo vyote vikiwa na thamani ya Sh59.65 milioni, mali ya kampuni ya Agritanza Ltd.
Walioshtakiwa wengine
Mbali na Ponda na Zainabu, washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Kuruthumu Mfaume, Zainabu Mohamed, Juma Mpanga, Farida John, Adam Ramadhan, Athuman Salim, Seleman Jumbe, Salum Mzee, Salum Ally na Rahma Amza.
Pia wamo Halima Abbas, Maua Omary, Fatihia Habibu, Hussein Ally, Shaban Ramadhan, Hamis Mohamed, Rashid Ramadhan, Yusuphu Penza, Alawi Mussa, Ramadhan Rashid, Omary Ismail, Salma Abdulatifu, Halid Issa, Said Rashid, Pesual Bakari, Issa Msuya na Ally Mohamed.
Wengine ni Mohamed Ramadhan, Abdallah Haule, Juma Hassan, Mwanaomary Makuka, Omary Bakari, Rashid Ndimbo, Hamza Ramadhan, Ayoub Juma, Maulid Nandepa, Bakari Jamal, Swalehe Abdul, Jumanne Mussa, Salum Abdallah, Hamis Mchomi, Bite Bilali, Amir Said, Juma Ally, Athuman Suleiman, Lukaiya Yusufu, Abubakari Juma na Ally Shaban.
Baada ya kuwasomea mashtaka, Kweka aliiambia mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kisha alitoa hati ya DPP inayozuia dhamana kwa Sheikh Ponda na watuhumiwa wenzake 49.
Wakili wa utetezi, Nassoro alipinga hati hiyo kwa madai kuwa sababu zilizotolewa na DPP za kuwanyima washtakiwa hao dhamana ni za kiujumla na kwamba mahakama haiendeshwi hivyo.
Wakili Nassoro alidai kuwa dhamana ya mtu ni haki ya msingi ya mshtakiwa, hivyo haiwezi kuondolewa kwa maelezo ya kiujumla."
"Makosa yote matano yanayowakabili wateja wangu yanadhaminika na kama DPP alikuwa anaona Ponda aondolewe kupewa dhamana ilibidi atoe sababu zinazoeleweka," alidai Nassoro.
Hivyo aliiomba Mahakama kutoa masharti ya dhamana kwa wateja kwake ambayo yanatekelezeka hususan kwa bibi kikongwe wa miaka 100.
Wakili Kweka alijibu hoja hizo kwa kusema kuwa kifungu cha 148 (4) kinajieleza chenyewe na kuwa DPP anapokitumia, mahakama inafungwa mikono na kwamba halazimiki kutoa sababu zozote.
"Ponda kwa sasa hapaswi kupewa dhamana kutokana na hati hiyo, atapewa dhamana hadi hapo DPP atakapoleta hati nyingine ya kutengua hati hii ya zuio la dhamana," alisisitiza Kweka.
Hata hivyo Hakimu Sanga alisema yeye yupo mahakamani kwa niaba ya mwenzake tu na kwamba hawezi kuamua chochote hadi hapo hakimu anayepaswa kuisikiliza kesi hiyo, Victoria Nongwa atakaporejea.
Aliiahirisha kesi hiyo hadi Novemba Mosi, mwaka huu itakapotajwa.
Baada ya kesi hiyo, Wakili Nassoro aliwaambia Waislamu kuwa suala hilo ni kweli limeleta hisia, lakini wajue limefika mahakamani hivyo watulie, wawe na subira na waamini kuwa mahakama itatenda haki.
Bakwata walaani
BARAZA la Waislamu Tanzania (Bakwata), limelaani matukio yote ya vurugu yaliyofanywa kwa makusudi na watu wanaotumia mwavuli wa dini ya Kiislamu na kutaka sheria ichukue mkondo wake ili haki itendeke.
"Sisi tunalaani vurugu. Tunataka watu wafuate sheria na waziheshimu," alisema Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Bakwata, Shaban Simba.
Simba aliongeza kusema: "Hatufahamu alichofanya Sheikh Ponda hata akakamatwa lakini kama amekamatwa kwa sababu ya vurugu, sheria lazima ifuate mkondo dhidi yake na wanaofanya vurugu hizo kwa mgongo wake."
Mihadhara marufuku
Katika hatua nyingine, Polisi wamepiga marufuku mihadhara ya aina yote nchini inayolenga kuleta uchochezi na kukashifu dini za wengine.
Akizungumza na Mwananchi jana, msemaji wa Polisi, Adivera Senso alisema polisi hawatamvumilia mtu au kikundi chochote chenye nia ya kuleta uvunjifu wa amani.
Senso alisema kuwa, kuna kikundi cha watu wachache kinachotumia mwavuli wa kidini kuvuruga amani ya nchi na kwamba jeshi hilo limejipanga kuhakikisha linakomesha vitendo hivyo.
"Napenda nikuhakikishie kwamba Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kuanza kuwashughulikia watu wote wanaohatarisha amani ya nchi hasa wale wanaoendesha mihadhara ya kidini na kutumia mwavuli wa kidini. Wote watadhibitiwa," alisema Senso.
Alisema kuwa kama mtu anataka kufundisha dini kwa kutumia mihadhara anatakiwa kufundisha maadili ya dini yake kwa waumini wa dini yake na siyo kukashifu dini za wenzake kwani jambo hilo linalenga kuleta uchochezi na uvunjifu wa amani.
"Polisi hairuhusu mikutano yote inayotumia lugha za uchochezi na wale wanaoendelea kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na kwamba hawaogopi vitisho vya mtu yeyote au kikundi chochote kinachojita cha kidini," alisema Senso.

0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....