Diva agwaya kuingia kwenye siasa, aambiwa yatamtokea ya Amina Chifupa



Unakumbuka kuna muda mtangazaji wa Clouds FM Loveness aka Diva alitangaza kuwa mwaka 2015 atagombea ubunge? Well, hakuwa anatania kwani hivi karibuni alianza kwa kuchukua kadi ya uanachama wa CHADEMA na kuandika kwenye website yake, “ts official!. Nimechukua Kadi ya Uanachama ya Chadema. 2015 Mungu akiniweka hai Inshaallah naingia katika Siasa Rasmi!. Thats what I want in life!. So hope gonna get support from my fans !. God Is Good!. In life chochote nipangacho huwa kinakuwa, Lets see. What future holds!. Special thanks to Patrick Bonge!. And my sisters!. Chadema all the wayyy.”


Diva akionesha kadi yake ya uanachama wa CHADEMA

Lakini pamoja na kuchukua uamuzi huo, jana Diva amesema amepewa vitisho kutoka baadhi ya watu kuwa hatofika popote na huenda yakamtokea kama ya marehemu Amina Chifupa.
“Kuna watu walinikalisha chini 4hours, wananiambia umemuona Amina Chifupa, kaishia wapi?! Basi niliogopa sana,” alitweet kumweleza mbunge wa jimbo la Kawe mheshimiwa Halima Mdee.
“Don’t tell me u give in so easily…..I thought i knew you…..kumbe mwoga?umenidisappoint!,” alisema Halima.
Mazungumzo na mheshimiwa Mdee yalimpa nguvu kidogo mtangazaji huyo ambaye aliandika, “Really?Basi Umerudisha imani yangu, Its official am in , Joining the movement , sitagive up tena,tatizo my friends hate politics.”

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter