SISTA ALIYEFUMANIWA AZUA BALAA JINGINE


WAKATI Mahakama ya Mwanzo  mjini Sumbawanga ikiwa imemtia hatiani  aliyekuwa mtawa wa Shirika la Kitawa la Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga, Sista Yasinta Sindani, kwa kufumaniwa na mume wa mtu na  kuamriwa kumlipa fidia  ya Sh 700,000 mlalamikaji, ameleta kizaazaa kwa mwanaume kwa kumdai talaka.
Mke wa Martin Msangawale , Asteria Mgabo akizungumza na  mwandishi wa habari hizi hivi karibuni alisema hukumu  iliyotolewa ameridhika nayo pia anadhamiria kufungua shauri   mahakamani hapo la kudai talaka.
“Baada ya hukumu kutolewa, nitaanza mchakato wa kufungua shauri mahakamani hapa kudai  talaka kwani siko tayari  tena kuendela kuishi na Martin,” alisema Asteria.
Wakati Asteria akisema hayo, habari zaidi zinasema mumewe Martin Msangawale, alikamatwa siku ya hukumu ya kesi hiyo wakati anajiandaa  kuingia  ndani ya mahakama kwa madai ya kujifanya afisa ardhi.
Akithibitisha habari hizo kwa mwandishi  wa habari  hizi, Mwanasheria wa Manispaa  ya Sumbawanga, Tulalemwa Mwenda  alisema ni kweli Martin amekamatwa.
“Martin alikamatwa  akituhumiwa  kujifanya  ofisa ardhi  wa manispaa  hii na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na upelelezi juu ya tuhuma hizo unafanywa na polisi,” alisema mwanasheria Mwenda.
Afisa mmoja wa polisi ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini kwa kuwa siyo msemaji alikiri kukamatwa kwa Martin na upelelezi juu ya madai kuwa alijifanya afisa ardhi na kujipatia fedha, unaendelea.
Martin hivi karibuni ilithibitishwa mahakamani mbele ya hakimu wa  mahakama  hiyo , Jaffar Mkinga kuwa alifumaniwa na Sista Yasinta katika nyumba moja ya kulala wageni iitwayo Chipa mjini hapa ambapo mwanamke huyo alitozwa faini ya shilingi 700,000.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter