Mahakama ya hakimu mkazi ya wilaya ya Musoma mkoani Mara imewahukumu maafisa wawili wa mamlaka ya mapato (TRA) kifungo cha miaka kumi na moja kila mmoja baada ya kupatikana na kosa la kushambulia.
Moja kati ya madhara waliyofanya watumishi hao. |
Maafisa hao wawili mmoja andaiwa kuwani ni mdogo wa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Meck Sadick.
Akisoma huku hiyo mwishoni mwa wiki hakimu Richard Maganga aliwahukumu maafisa hao ambao ni Sadick Salum na Mussa Msangi, kufuatia kukiri kosa la kujeruhi, kudhuru mwili na shambulio la kawaida ambalo walitenda novemba 10/2012 katika hoteli ya Sentavin mjini hapa.
Maganga alisema kuwa watuhumiwa walifanya kosa hilo kinyume na kifungu namba 225 sambamba na kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka2002.
Alifafanua makosa matatu waliyofanya kwa pamoja kuwa kosa la kwanza ni kujeruhi ambalo adhabu yake ni miaka mitano kila mmoja , kosa la pili ni kudhuru mwili ambalo nalo pia adhabu yake ni miaka mitano kwa kila mmoja na kosa la tatu ni shambulio la kawaida ambalo adhabu yake alisema ni mwaka mmoja kila mmoja hivyo adhabu hizo zikwenda sambamba kwa kutumikia miaka sita jela kila mmoja. Hakimu alisema kuwa washitakiwa hao wote wawili watatumikia kifungo hicho ili liwe fundisho kwa watu wenye tabia za aina hiyo mkoani hapa.
Kwa upande wake mwendesha mashitaka wa polisi Fransisi alisema kuwa washitakiwa hao kwa pamoja waliowashambulia na kuwajeruhi Edgar Mapande, Witness Leonard na Doris Mayuki katika hoteli ya Sentavin Novemba 10 mwaka huu.
Baada kutolewa kwa adhabu hiyo ambayo ilivuta mamamia ya wananchi wa Manispaa ya Musoma kutokana na watuhumiwa hao kutamba mitaani kuwa kuwa kamwe mahakama hiyo haiwezi kuwafunga kwa uwezo wao wa fedha na mahusiano ya kindugu na baadhi ya viongozi serikalini, Sadick akimgombeza hakimu kwanini aliuamua kumkomoa kwa kupata kifungo hicho.
“Umeamua kunikomoa kama haonijui eti haya tutaona lazima nitatoka hapa si mwisho wa maisha yangu” alisikika Sadick akimwambia hakimu huku akiwa ameshika mikono mfukoni.
NJE YA MAHAKAMA.
Baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo baadhi ya ndugu wa watu walijeruhiwa na wananchi waliokuwa wakishuhudia baadhi ya vitendo vya kinyama na kibabe vilivyokuwa vikifanywa na maafisa hao walisikika wakisema kuwa mahakama hiyo imetenda haki kwani licha ya kuwa ni masikini lakini haikuangalia uwezo wa watumiwa kifedha na kutoa adhabu kulingana na sheria.
Ni sehemu tu ya majeraha yaliyosababishwa na maafisa hao kwa tukio la November 10. |
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....