WAWILI MBARONI KWA KUINGIA NA BASTOLA ZANZIBAR...

                   Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa

Watu  wawili wamekamatwa na silaha katika bandari ya Zanzibar wakati wakitokea Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alisema watu hao walikamatwa na bastola aina ya cz 92 ikiwa na risasi nane wakati wakitokea Dar es Salaam kwa boti ya Kilimanjaro 4.

Alisema baada ya wahatumiwa hao kuhojiwa walieleza kuwa ni wamiliki halali wa silaha hiyo, lakini Kamanda huyo alisisitiza kuwa sheria ya watu kumiliki silaha haitumiki  Zanzibar.

Alisema watu hao watafikishwa mahakamani. Aliwataja kuwa ni Daudi Obeto Matiku (40) na Emanual Joseph Obeto (35).

Hatua hiyo imekuja baada ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha ulinzi na usalama ili  kupambana na wahalifu.
 
CHANZO: NIPASHE     

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter