Msanii wa filamu na muziki nchini, Shilole amefunguka kwa kusema anafanya muziki wa kucheza na wanaume jukwaani ili kukidhi mahitaji ya aina ya burudani wanayoihitaji watu wake.
Akizungumza na Bongo5 leo akiwa Moshi, Shilole amesema anafanya muziki kulingana na mahitaji ya mashabiki wake na si kwa kusikiliza mawazo ya mtu mmoja mmoja yasiyokuwa na manufaa kwenye muziki wake.
“Nafanya muziki anaofanya Shilole peke yake,na wapenzi wengi wa muziki wangu wanafurahishwa na kitendo cha kuwapandisha vijana na kucheza nao, hii inaleta mzuka kwangu na kwa wapenzi wa burudani,” amesema.
“Ninavyowapandisha vijana na kucheza nao huku wamenishika au tumeshikana ndio wanaona hatari? Mbona ni mambo ambayo yanafanyika kwenye show mbalimbali, pia ili kuleta uhalisia wa show ni lazima mshikane kidogo,kwa wale ambao wanaona kama naharibu ni washamba tu.”
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....