Ajali mbaya nyingine imetokea usiku huu katika mlima kwa Kitonga wilaya ya Kilolo mkoani Iringa katika barabara kuu ya Dar es Salaam -Iringa .
Katika ajali hiyo watu wawili wamekufa papo hapo huku
watu wawili wakijeruhiwa vibaya baada ya malori mawili kugongana uso kwa uso .
Ajali hiyo imetokea mida ya saa 12.50 jioni ya leo ikiwa ni dakika takribani 30 baada ya ajali ya basi la JM kupinduka eneo la Mazome wilaya ya Kilolo.
Basi la JM lilipinduka mida ya saa kumi na mbili na dakika 20 na kujeruhi watu 15
Chanzo ni dereva wa lori la IT lililokuwa likisafirishwa kwenda nchi za kusini mwa Tanzania aliyekuwa akitaka kulipita gari la mbele mlimani na katika kona kali .
Dereva wa lori hilo la IT aliyetambuliwa kwa jina la Gody amevunjika mguu wake na dereva na utingo la fuso wamekufa papo hapo huku mwanamke aliyekuwa katika lori la IT akisalimika .
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....