WATOTO wawili wa familia moja wamekufa maji baada ya kutumbukia kisimani walipokuwa wakichota maji wilayani Bunda, mkoani Mara.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea juzi majira ya saa 3:00 asubuhi, katika Kijiji cha Changuge Kata ya Mcharo wilayani hapa, wakati watoto hao walipokuwa wakichota maji kisimani.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mcharo, Waziri Kingi aliwataja watoto waliokufa maji kuwa ni Daud Makoye (4) na Raphael Makoye (2). Walikuwa wanaishi nyumbani kwa Onesmo Mashenene mkazi wa kijiji cha Changuge.
“Wakati Raphael akichota maji alitumbukia ndani ya kisima hicho, mkubwa wake yaani Daud alipojaribu kumuokoa wote wakazidiwa maji na kupoteza maisha,” alisema. Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Ferdinand Mtui, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba upelelezi bado unaendelea.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....