Sababu za vurugu.
• Tarehe 24/4/2013 ulikuwa ufanyike uchaguzi wa mwenyekiti wa kijiji, mgombea wa Chadema alienguliwa na Afisa mtendaji wa kata ambaye ndiye alikuwa msimamizi wa uchaguzi.
• Chadema wakakata rufaa, rufaa yao ikatupwa na msimamizi wa uchaguzi (Afisa mtendaji).
• Akaamua ufanyike uchaguzi wa kitongoji, Chadema wakashinda, wananchi wakataka ufanyike na uchaguzi wa kijiji ili wapate mwenyekiti wao.
• Leo ccm wakataka kuweka mwenyekiti wao wa kijiji ambaye hakuchaguliwa na wananchi.
• Wananchi hawamtaki mgombea wa ccm ambaye amepitishwa kwa nguvu baada ya kuenguliwa kwa Bw Maliwa wa CdM.
• Wananchi wakaamua kuvamia kwenye kikao ambacho mwenyekiti wa kuchonga wa ccm alikuwa ana kabidhiwa ofisi kinyemela pasipo kuchaguliwa na kutangazwa kwenye mkutano mkuu wa kijiji.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....