SKENDO: WANAWAKE WEZI WANASWA SUPERMARKET WAKIIBA BIDHAA NA KUFICHA KWENYE NYETI ZAO(SEHEMU ZA SIRI)....!!

Kimabu-300x300[1]

Wanawake wawili kutoka mji wa Kiambu, Central Province, Kenya walibambwa na walinzi wa supermarket wiki iliyopita, wakiwa na lita tano za mafuta ya kupikia kati ya mapaja yao. Wanawake hao, inasemekana ni baadhi ya wahusika katika genge maarufu la uibaji madukani (shop lifting)

kwa mujibu wa utawala wa supermarket hiyo, wamekua wakiibiwa sana, kitu kilichowalazimu kuweka video camera ya ulinzi (CCTV) ili kupunguza wizi huo. Miezi michache tu iliyopita, mwanamke aliyevaa baibui alikamatwa na bidhaa zenye thamani ya maelfu ya shilingi (Kenyan shillings) akiwa amezificha ndani ya nguo zake.
Wanawake hawa wawili, siku yao ya arobaini iliwadia walipoamriwa warudi ndani na walinzi wakati wakijaribu kuondoka kutoka kwenye supermarket hiyo. Walijaribu kujikausha ili wasishtukiwe lakini ilikua too late maana walinzi walishajua wanawake hao wana vitu gani kati ya mapaja yao.
Walikamatwa na kufungwa kamba kama mbuzi kwenye lango la kuingilia kwenye supermarket hiyo, na kulazimishwa kufunua sketi zao ili walichoiba kionekane kwa watu wote wanaoingia kwenye supermarket hiyo. Haijajulikana kama dhumuni lilikua kuwaaibisha, kuitaarifu jamii kwamba hawa ni wezi, kutoa fundisho kwa vibaka wengine, au vyote. Walishikiliwa hapo mpaka polisi walipowasili na kuwachukua

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter