Pichani juu ni nyoka lakini si yule aliyemng’ata Jengua.
Akizungumza na mwandishi wetu nyumbani kwake Magomeni Mapipa, Dar Jengua alisema hivi karibuni aling’atwa na nyoka huyo porini wakati akijiandaa kushuti hivyo kupata jeraha mguuni lililosababisha ashindwe kuendelea na kazi hiyo.“Nilipata maumivu makali sana hadi ikabidi tuahirishe kuigiza filamu ya Big Mama Afrika lakini baada ya kuchanjwa na kuwekwa dawa ya ‘jiwe la nyoka’ nilipata nafuu kidogo ila kwa sasa naendelea vizuri,’’ alisema Jengua.
Kabla ya tukio hilo, staa huyo alipata ajali nyingine ya kuteleza mtoni na kuangukia jiwe, hali iliyosababisha azirai kwa muda wa saa mbili kabla ya kupatiwa matibabu.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....