MAHAKAMA  ya Juu Kabisa nchini Kenya imeamua leo kuwa Uhuru Kenyatta alichaguliwa  kwa haki kuwa Rais wa nne wa nchi hiyo, na kutupilia mbali pingamizi  lililowekwa na mgombea Raila Odinga aliyedai kwamba kura  zilichakachuliwa na mashine za uchaguzi zilijaa kwikwi.
Uamuzi huo umesafisha njia kwa Uhuru Kenyatta kuingia Ikulu. Anatarajiw kuapishwa wiki ijayo kwenye Machi 9, 2013 hivi.
“Ni  uamuzi wa mahakama hii kwamba walalamikiwa wa tatu na wa nee  walichaguliwa kwa haki”, alisema Jaji Mkuu wa Kenya Willy Mutunga,  akimaanisha Kenyatta na mgombea mwena na Naibu Rais William Ruto  wameshinda kihalali.
Jaji  Mkuu huyo alisema mahakama imetekeleza wajibu wake katika muda huo wa  kihistoria. “Sasa ni juu ya Wakenya, viongozi wao, taasisi za kijamii,  sekta binafsi na vyombo vya habari kutekeleza wajibu wao kuhakikisha  umoja, amani, utaifa na maendeleo ya taifa vinahifadhiwa”, aliongezea.
Rais mteule wa Kenya huyo alimshinda mpinzani wake kwa asilimia 50.07 dhidi ya asilimia 43,28 za Odinga.
CREDIT: MPEKUZI HURU 



0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....