"NATAFUTA MUME AMBAYE HATANIBANA KUTAFUTA PESA"....SNURA



MSANII wa filamu na muziki mwenye mvuto wa aina yake Snura Mushi ‘Snura’, ameamua kutoa la moyoni kwa madai kuwa sasa anatafuta mwanaume wa kuweza kufunga naye pingu za maisha lakini kwanza kabisa akubali kumpa muda mrefu wa kutafuta pesa ili asiwe tegemezi baada ya kuingia ndani ya ndoa hiyo.

Kauli ya msanii huyu imekuja mara baada ya mwandishi wetu kumswalika  maswali  kadhaa  kuhusiana  na  mikakati  ya maisha  yake  ya  muziki  na  mahusiano .....
Akiongea  kwa  mbwembwe, Snura  alidai   si kwamba hataki kuolewa bali hataki kuishi ndani ya ndoa na kuwa tegemezi kwa mwanaume.

“Sitaki kuishi na mwanaume kabla hajakubali kunipa muda wa mimi kutafuta pesa...
 Najua anaweza kuwa na uwezo wa kila kitu lakini hivyo vyote vitakuwa vya kwake na mimi natakiwa kuwa na mali zangu, lakini bila hivyo nitazeekea kwangu,” alisema.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter