MSANII RADO ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUPOKEA KICHAPO KIKALI KUTOKA KWA WAHUNI MWANANYAMALA....!!



MSANII wa muziki na filamu Bongo, Saimon Mwapagata ‘Rado’ amenusurika kifo kutoka kwa vijana waliofunga njia maeneo ya Mwananyamala, jijini Dar Jumapili iliyopita.
Kwa mujibu wa rafiki wa Rado ambaye pia ni msanii wa filamu, Deogratius Shija, tukio hilo lilitokea usiku wakati Rado alipokuwa akirudi nyumbani kwake
“Alikuta njia imefungwa na vijana watatu, alijaribu kuwapigia honi lakini hawakufungua njia.
“Rado alishuka kwenye gari na kuwauliza kwa nini wamefunga njia wakamjibu kwamba mmoja wao ameibiwa simu, hivyo wanamtafuta mwizi wao.
Shija alisema kwamba ghafla vijana wale walimvamia Rado  na kumshushia kipigo cha haja wakiwa na mapanga na marungu na kumjeruhi hadi akapoteza fahamu.
 “Nilipigiwa simu na msamaria  na kuambiwa kuwa Rado hajiwezi, sababu kuna watu wanaomjua maeneo yale alipelekwa Oysterbay Polisi kisha kukimbizwa Hospitali ya Mwananyamala ambako alishonwa, kifuani na mguuni,”

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter