BINTI wa miaka saba (jina tunalihifadhi kwa sababu maalum), amefanyiwa ufirauni wa kutisha baada ya kijana mmoja wa kiume aliyetambulika kwa jina moja la Justin kudaiwa kumuingilia kimwili na kumharibu vibaya sehemu za siri kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo.
Akisimulia mkasa huo wa kusikitisha, binti huyo anayesoma darasa la pili katika shule moja iliyopo Sanawari jijini hapa, alisema kuwa mara ya kwanza alipelekwa nyumbani kwa mwanaume huyo na msichana mmoja ambaye kiumri ni mkubwa kuliko yeye (jina lake linahifadhiwa).
“Alikuwa ananipa pipi kisha ananipaka mafuta na kuni… (anaeleza alichokuwa anafanyiwa). Mara kwa mara alikuwa ananisubiri njiani ninapotoka shuleni na kunipeleka chumbani kwake,” alisema binti huyo mdogo kwa masikitiko.
Mwanaume mmoja aliyekuwa miongoni mwa walioshtukia mchezo huo, amesema baada ya majirani kumuona mtoto huyo akiingia mara kwa mara kwenye chumba cha Justin anayesoma kidato cha nne kwenye shule moja ya sekondari jijini hapo, walienda kumtonya mama yake anayemlea mtoto huyo peke yake baada ya mumewe kuoa mke mwingine.
“Mama yake alipomchunguza mwanaye, alishtuka sana kwa jinsi alivyokuwa ameharibika, akampeleka hospitali ambapo daktari alimchukua vipimo na majibu yalipotoka, ilithibitika kuwa ni kweli mtoto huyo amekuwa akifanyiwa ukatili huo kwa kipindi kirefu.
Baada ya taarifa hizo kulifikia jeshi la polisi, kijana huyo alikamatwa na kupelekwa kwenye Kituo cha Polisi cha Mjini Kati alikofunguliwa kesi.
Hata hivyo, katika hali iliyozua utata, Justin alitolewa kinyemela kituoni hapo na baadaye ikadaiwa kuwa wazazi wa binti huyo na wazazi wa Justin, walifikia makubaliano ya wazazi wa mtuhumiwa kulipa kiasi cha shilingi laki saba kama fidia.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....