Mkali wa vina na mashairi kutoka pande za Ilala anayefahamika kwa jina maarufu la 'Chid Benz' ameanza kupata sifa mbaya baada ya kumpiga mwanamuziki mwenzake 'Ngwea' nje ya ukumbi wa Ambassador Lounge ulioko kwenye jengo la Benjamini Mkapa tower Posta usiku wa kuamkia Machi 22.
Kupigwa kwa 'Ngwea' kulikuja baada ya 'Chid' kumzingua 'Dully' alipokua akiingia ambapo mwisho wake aliamua kuondoka.
Alipoondoka 'Dully', 'Ngwea' akamuuliza inakuaje unamzingua kubwa lao, ndipo 'Chid' alipopaniki na kuanza kutoa lugha chafu huku akitaka kutokumsikiliza 'Ngwea', inasemekana 'Ngwea' aliamua kukaa kimya lakini 'Chid' aliendelea kungea kwa hasira na kusema "ndio nimemzingua kwani yeye nani" na kumbadilikia 'Ngwea'.
'Ngwea' aliamua kuondoka kwenye ukumbi huo lakini alipofika chini ya ghorofa ndipo 'Chid' alipomfuata na kuanza kumshambulia mwanamuziki mwenzake huyo na baadaye kumjeruhi kwa chupa mkononi.
Lakini baada ya hapo 'Ngwea' aliweza kufika hospitali na kuweza kupatiwa matibabu ya jeraha hilo la chupa.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....