KATIKA hali isiyo ya kawaida, mastaa wa kike ndani ya Bongo Movies, waligoma kuosha vyombo katika msiba wa Juma Kilowoko ‘Sajuki’, Ijumaa Wikienda lilishuhudia.
Mgomo huo ulioleta tafsiri mbaya kwa mastaa wa kike, ulitokea Januari 4, mwaka huu nyumbani kwa marehemu Tabata-Bima jijini Dar mara baada ya taratibu za maziko kukamilika.
Mama Abdul ambaye ni mwigizaji mkongwe, aliwataka wasanii wa kike wainuke wakaoshe vyombo pasipo kuhofia kuharibu kucha zao za kubandika lakini wachache walitii huku wengi wao wakiendelea kung’ang’ania viti.
Mastaa ambao walionesha kushiriki kazi mbalimbali msibani hapo siku hiyo ni Salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’, Koleta Raymond ‘Coletha’, Suzan Lewis ‘Natasha’, Yvone-Cherry ‘Monalisa’ na Jacqueline Wolper.
Sajuki alifariki dunia Januari 2, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matatizo ya muda mrefu ya saratani ya ngozi, uvimbe tumboni na upungufu wa damu.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....