MSANII mahiri wa filamu Irene Uwoya, ameamua kuweka wazi kuwa safari yake aliyowahi kuifanya ya nchini Uingereza mwaka jana kwa ajili ya mazungumzo ya kufanya filamu ya kimataifa bado hayajazaa na matunda na hadi sasa wapo kwenye mazungumzo.
Kauli ya msanii huyo ilimfanya mwandishi wa DT kumdadisi zaidi, ambapo alisema kuwa kwa sasa kitu wanachokizungumzia ni namna watakavyoandika story ingawa hakutaka kuweka wazi ni story ya namna gani.
Hata hivyo alisema kuwa bado hawajafikia mazungumzo ya kulipwa kiasi gani na lini watafanya lakini anaamini kila kitu kitakuwa safi kwani watu hao wameonesha nia ya kufanya nae kazi.
Pamoja na hayo alishindwa kuwaweka wazi watu hao hata kwa kuwataja majina, kwa madai kuwa kwa sasa siyo wakati wake kwani muda ukifika mashabiki wake watajua anaenda kufanya kazi na kampuni gani.
“Bado tunaendelea na mazungumzo najua watu wanasubiri kuona ukweli juu ya maneno yangu haya lakini nachotaka kusema ni kwamba ni kweli nilienda kwa ajili ya mazungumzo ila bado mambo hayajakaa sawa,” alisema Uwoya
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....