PICHA YA MSANII ‘ROSE NDAUKA’ NA ‘TIMBULO’ WAKIWA KITANDANI YAZUA UTATA MKUBWA…!!

http://dartalk.com/wp-content/uploads/2013/01/timbulo_ndauka.jpg

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Timbulo, ameonekana kuvuta hisia za watu wengi kwenye mitandao ya kijamii na kuacha maswali mengi baada ya kuonekana akiwa na msanii wa filamu Rose Ndauka kwenye pozi tata chumbani huku Ndauka akiwa amevaa taulo na hapo ndipo utata huo unapokuja.


Timbulo kutokana na picha hiyo inachora ramani tata, ambayo itamweka kwenye wakati mgumu kutokana na mashabiki wake wengi kuhisi walikuwa kwenye hisia kali za mapenzi hasa uvaaji wa taulo wa Ndauka tena wakiwa kitandani.

DarTalk baada ya kupata picha hiyo ilimtafuta Timbulo na kuzungumza naye ambapo, alidai kuwa picha hiyo imepigwa wakati wakishuti filamu ambayo wao wote wameshirikishwa na hapo hakuna ubaya wowote ulifanyika.

“Dah nashindwa kueleza kwani picha ni kweli tulikuwa chumbani na hakuna kitu kilichotokea zaidi amani tu, na nachoweza kusema watu walihisi mimi natoka na Ndauka ila siyo hivyo ingawa nampenda sana huyo dada,” alisema.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter