MUUAJI WA MWANGOSI AUGUA GHAFLA!!

Kushoto ni muuaji wa Mwangosi (kushoto) akijiandaa kumfyatulia Bomu,
picha ya kulia ni yeye ktk pozi.
WAKATI jamii ikiendelea kufuatilia kesi ya mauji ya aliyekuwa Mwandishi Habari wa kituo cha Chanel Ten Mkoani Iringa Daud Mwangosi Mtuhumiwa wa mauwaji ya mwandishi huyo Askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha kuzuia na kutiliza Ghasia (FFU) mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23)leo ameshindwa kufika mahakamani katika kesi yake baada ya kudaiwa kuwa ni mgonjwa .
Kitendo cha Askari huyo kudaiwa kuwa ni mgonjwa imekwamisha Kesi hiyo ambayo leo ilitarajiwa kutajwa tena Mahakamani hapo.

Mwendesha mashtaka wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Adolf Maganda aliieleza Mahakama mbele ya Hakimu wa Mahakamani ya Kakimu Mkazi Wilaya ya Iringa Dyness Lyimo kuwa mtuhumiwa alipaswa kufikishwa Mahakamani hapo.

Mwendesha mashtaka huyo alimuomba Hakimu kupangwa tarehe nyingine ya kutajwa kesi hiyo ambayo bado upelelezi wake haujakamilika.Hakimu Lyimo aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 31 itakapotajwa tena .

Mtuhumiwa huyo anatuhumiwa kumuua kwa makusudi kwa bomu aliyekuwa mwandishi wa habari wa Chanel Tena mkoa wa Iringa marehemu Mwangosi Septemba 2 mwaka jana katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa wakati wa vurugu kati ya polisi na wafuasi wa Chadema .kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai. Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter