Morogoro: Mwanafunzi wa darasa la pili amchoma mwenzie kisu!!


Picture

RAIA wa Kata ya Mafiga mjini hapa wamewatupia lawama walimu wa Shule ya Msingi ya Mafiga ‘B’ kwa kuzembea na kusababisha mwanafunzi wa darasa la pili kuingia darasani na kisu kila siku kisha kuwachoma wenzake.

Uchunguzi wa mwahabari wetu ulibaini kuwa kufuatia kitendo hicho, wazazi wenye watoto wanaosoma shuleni hapo wanakusudia kuitisha kikao cha wazazi ili kujua sababu za walimu hao kuruhusu mwanafunzi huyo (jina linahifadhiwa) kuingia darasani na kuwajeruhi wenzake.

Wikiendi iliyopita mtoto huyo aliingia darasani na kisu kisa kumchoma mwanafunzi mwenzake (jina linahifadhiwa) usoni ambapo ililazimu kushonwa zaidi ya nyuzi 7.

Akizungumzia tukio hilo la kutisha, mazazi wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Lydia alithibitisha mwanaye kufanyiwa unyama huo.

Ilielezwa kuwa ukiacha matukio ya aina hiyo ya siku za nyuma, wiki mbili zilizopita alimchoma mwanafunzi mwingine wa kike lakini wahusika wamekuwa wakijidai ‘kupotezea’ bila kujua kwa nini mtoto huyo anafanya hivyo.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter