WANAFUNZI wawili wa chuo cha biashara wamepoteza CBE
wamekufa papo hapo kwenye ajali baada ya kugonga tela la mizigo
lililokwama barabarani baada ya kuhalibika.
Ajali
hiyo ilitokea jana majira ya saa 1.00 usiku baada ya kugonga tela la
lori la mizigo kwa nyuma wakati wanafunzi hao walipokuwa wakitokea
kwenye mwaliko wa sherehe ya rafiki zao iliyofanyika katika kijiji cha
ihumwa manispaa ya Dodoma.
Gazeti hili
lilishuhudia msongamano mkubwa wa magari katika barabara hiyo iliyopo
pembezoni mwa kambi ya jeshi ya Ihumwa kwa takribani saa zaidi ya tatu
kabla ya polisi wa usalama barabarani kufika na kuongoza utaratibu wa
kuondoka.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa
wa Dodoma Suzan Kaganda alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa
wanafunzi hao wakati wakiendesha pikipiki hiyo yenye namba za usajili T
420 CCN waliokuwa wakukitokea barabara ya morogoro kuingia mjini.
Suzan
aliwataja kuwa ni Ramadhan Lesso na Gerger Lwandala wanafunzi wa CBE
na kwamba uzembe wa Dereva wa lori hilo lenye namba za usajili T 477 ABM
na huku Tela lake ni T 838 AAZ aliyeliacha barabrani zaidi ya wiki bala
kuweka alama yoyote huku matengenezo ya barabara hiyo yakiendelea katik
eneo hilo.
Aliongeza kuwa miili ya
marehemu hao iliyokuwa imehalibika vibaya kutokana na kufumuka fuvu la
kichwa cha aliyekua dereva wa pikipiki hiyo na ubongo kusambaa katika
eneo hilo imehifadhiwa katika hospital ya mkoa.
Kwa picha za ajali hiyo bofya soma zaidi
lakini tunaomba radhi kwa picha hizo zinaleta usumbufu ukiziangalia
Miili ya Marehemu Ramadhan Lesso na Gerge Lwandala inaonakana kabla ya kuondolewa katika kijiji cha Ihumwa barabara ya Morogoro Dodoma kabala ya kuondolewa na kuhifadhiwa katika chumba cha maiti hospital ya mkoa.
Baadhi
ya watu wakiisogeza miili ya Wanafunzi wa CBE Dodoma walikufa kutokana
na kuligonga tela la lori kwa nyuma kutokana na mwendo kasi huku lori
hilo likiwa limetelekezwa zaidi ya wiki bila alama yoyote barabarani
hapo.
Baadhi
ya asikari wa Jeshi la wananchi walionekana kujaribu kutoa msaada
katika ajali hiyo iliyosababisha vifo vya wanafunzi wa chuo cha biashara
CBE Dodoma.
Asikari
wa wasalama barabarani akisaidiana kupima upana wa barabara sehemu
ilipotokea ajali hiyo ilihusisha pikipiki na lori la mizigo.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....