Kwa kukumbusha tu, Emma ni binti aliyefukuzwa shule kutokana na ujauzito. Ujauzito wa Emma ulikuja baada ya kufanyiwa kitendo cha ukatili cha ubakwaji.
Kwa mdomo wake mwenyewe, Emma
ameelezea hali halisi na kusema kwamba hakupenda huo ndio uwe
mustakabali wake wa maisha kwa kuwa alikuwa na ndoto nyingi sana katika
maisha. Emma hakupenda kubakwa.
Tukio hilo limemkosesha nafasi ya kupata haki yake ya msingi, elimu. Emma katika maelezo yake anasema elimu ndio ingemsaidia katika maisha yake yeye na mwanae.
Akiwa na namba yake ya mtihani tayari kwa ajili ya
kufanya mtihani wa kidato cha nne 2013, Emma alisubiria kwa hamu majibu
ya ombi lake kwa Wizara ya Elimu imruhusu kufanya mtihani huo. Hata
hivyo, Emma hakuweza tena kufanya mtihani kwa kuwa hakupewa ruhusa ya
kufanya hivyo.
Kupitia Wanawake Live, Waziri wa Sheria na Katiba Mhe Mathias Chikawe amezungumza na kueleza sheria ikoje katika masuala kama haya, na kumalizia kuwa 'Hakuna mimba za bahati mbaya'.
Kupitia Wanawake Live, Waziri wa Sheria na Katiba Mhe Mathias Chikawe amezungumza na kueleza sheria ikoje katika masuala kama haya, na kumalizia kuwa 'Hakuna mimba za bahati mbaya'.
Waziri, Chikawe
Maswali ambayo wengi wanajiuliza ni pamoja na Je, sheria inayotumika kuongoza elimu nchini Tanzania, inawanufaisha wananchi au ni sheria iliyowekwa kukandamiza kikundi fulani cha watu?
Je, Emma Roberts hakupaswa kupigania haki yake ya kupata elimu eti kwa sababu Mhe Waziri wa Sheria na Katiba amesema kwamba 'Hakuna mimba za bahati mbaya'?
Tupia maoni yako hapo chini......
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....