Mwanafunzi aliyejinyonga baada ya kufeli mtihani wa kidato cha nne...
|
Khamis Mkundo Kijana aliyejinyonga. |
MADENTI wa Shule ya
Sekondari Sabasaba na Kituo cha Krelluu mjini hapa wamemlilia mwenzao,
Khamis Mkundo aliyejinyonga kwa hofu ya kufeli mtihani wa taifa (Necta)
wa kidato cha nne, mwaka huu.
|
\Hii ndo barua ya Khamis Mkundo aliyoiacha kabla ya kujinyonga. |
Denti huyo, mkazi wa Mwangata C mjini hapa aliwaliza wenzake aliokuwa
akisoma nao Sabasaba na baadaye kwenye kituo hicho ambapo alikuwa
‘akiristi’ baada ya kufeli mtihani huo zaidi ya mara moja.
|
Wana usalama wakisoma barua aliyoiacha denti huyo. |
“Inauma sana, marehemu alikuwa akijitahidi sana kusoma, tuliweka
mikakati ya pamoja ili tuweze kufanya vizuri mwaka huu lakini ghafla
tukasikia amejiua,” alisema mwanafunzi mmoja ambaye hakutaka jina lake
liandikwe gazetini.
Jamaa huyo alijiua Jumapili iliyopita kwa
kujinyonga kwa kamba na kuacha barua ndefu iliyosomeka kuwa amefanya
hivyo si kwa kupenda, ila alichukizwa na hatua yake ya kufeli mara kwa
mara akajiua ili kuepuka aibu hiyo.
'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....