Marehemu Hamida Urembo |
Hamida na mumewe yahaya walibahatika kupata mtoto wa
kike mwenye miaka mitatu sasa.Kwa mujibu wa dada wa Hamida ndoa yao
ilikuwa ya misuko suko sana.Mume alikuwa sio mwaminifu mara nyingi
alikuwa akizini nje.Ukiacha hilo alikuwa akimpiga sana mkewe mpaka
kumzimisha.
Matatizo ambayo ndugu walikuwa wakiyajua na
walishasuluhisha mara nyingi na Hamida kurudi kwa mume kuendelea na
maisha.Hii ya mwisho ndio ilikuwa kubwa zaidi.Mume alikuwa akimtongoza
housegirl hapo nyumbani na alipokuwa kesho housegirl akamfahamisha mama.
Akamueleza jinsi gani muwewe amekuwa akimsumbua
kumtaka kimapenzi.Hamida akamwambia
anataka tu uthibitisho kama ni kweli.Siku ya siku Yahaya akamlazimisha
Hamida kwenda kwao na Hamida akakubali akijua kuna jambo.Akasindikizana
na mumewe mpaka kituoni mume akijua mkewe hayupo kumbe mke aligeuzia
njiani akarudi nyumbani akajificha chini ya uvungu chumbani kwa
housegirl wake.Baadae mume akawasilia na housegirl kuwa anarudi
nyumbani,aliporudi akaendelea kuomba mambo tena akavua nguo kabisa
akabaki na boxer.Wakati huo yupo chumbani kwao na mkewe.Housegirl
akamwambia wahamie chumbani kwako hapo sio salama.Basi wakahamia
chumbani na akawa ndio anamuinamisha dada ili amfanye Hamida akatoka
chini ya uvungu ili kumuokoa dada na kumuonyesha mumewe kuwa alikuwepo
na amejua usaliti wake.Na alipokuwa chini ya uvungu alikuwa akirekodi
kila kitu kwenye simu na alipotoka na picha akapiga.
Huyu ndiye Yahaya aliyekuwa mume wa marehemu Hamida |
Hamida alitoka
hapo akashitaki kwao na kwao wakamwambia aende kwa mjomba wa mumewe
kumueleza matatizo ya mtoto wao. Alipofika kwa mjomba akaambiwa wanaume
ndivyo walivyo avumilie tu arudi kwa mumewe.
Hamida
akarudii kwao akiwa hana hana raha lakini uamuzi aliouchukua ni kuachana
na mumewe kwani alikuwa kashachoka. Wakawa wakivutana sana mume
akimsihi arudi nyumbani walikokuwa wakiishi Mbagala ila Hamida
hakuridhia.
Hamida alishaenda mpaka Bakwata ili mumewe aamriwe kutoa talaka.
Mwisho wa Hamida kuonekana nyumbani ni siku ambayo
yeye na ndugu zake walikuwa waende kijijini kwao kwenye viwanja
walivyopewa na babu yao.Ila siku hiyo Hamida alitoa udhuru kuwa haendi
na akamtaarifu mama yake kuwa Yahaya kamuita akachukue vitu vyake
vilivyobakia.Mama akamkatalia kwenda
akamwambia kuna kaka zake wakubwa aache wataenda kuvifata kwani huyo
mume ni mshenzi anaweza kumfanyia kitu kibaya.Hamida akamwambia mama
anataka kwenda mwenyewe kwani kuna vyeti vyake muhimu akavichukue.
Basi mama akamuacha aende kishingo upande lakini mama
akamwambia basi nenda hata na mdogo wako.Akaenda na mdogo wake lakini
kufika kule mume akamkatalia mdogo mtu kuingia ndani.
Wakabishana sana kwa nini asiingie mdogo mtu kuepusha shari akaenda kukaa kwa jirani
asubiri kuitwa. Akakaa na muda kupita kukawa kimya akajua wale wameelewana ndio maana hakuna makelele hivyo akaendelea kusubiri.
Akakaa weee mpaka jioni giza lilipoanza kuingia kidogo
Yahaya akampigia simu kwa kutumia simu ya Hamida akimwambia aondoke tu
arudi nyumbani wao wameshaondoka na vyombo wamebeba.
Mdogo mtu akaondoka kurudi nyumbani kwao Tabata akijua mke na mume wameelewana kumbe dada yake ameshakufa ndani.
Mdogo mtu akafika nyumbani saa mbili usiku na
kumwambia mama jinsi Hamida alivyomuudhi kamuacha yeye kwa jirani na
akaondoka na mumewe Yahaya.Mama
machale yakamcheza akanyanyua simu akampigia Yahaya kumuuliza mwane yupo
wapi.Yahaya akamjibu kuwa ameachana nae kitambo mama akamwambia sio
kweli mwanangu hawezi kuchelewa kurudi nyumbani na hana kawaida
hiyo.Yahaya akamjibu atarudi tu Hamida mtu mzima.
Mamam tayari alishajua kuna jambo akampigia simu baba
Hamida aliyekuwa Arusha kumtaarifu kilichotokea. Baba Hamida akampigia
Yahaya lakini hakupokea simu.Wasiwasi ukazidi kutanda na ndugu kupeana
taarifa zaidi.Asubuhi kulipokucha wakaenda Mbagala kwa Yahaya lakini
wakatoa taarifa polisi.Polisi wakawaondoa wasiwasi kwamba hao wanajuana
wenyewe labda wameamua kukumbushiana.
Ndugu hawakuridhika wakaenda kwa mjumbe awaruhusu
wavunje nyumba waingie ndani
pengine kamfungia ndani maana ilikuwa kawaida yake kufanya hivyo
kumfungia Hamida ndani.Basi mjumbe akaruhusu mlango uvunjwe walipoingia
ndani palikuwa patupu hawakuona kitu wala dalili za mauaji.Kuna chumba
ambacho ni stoo hicho walishindwa kufungua na mjumbe akawaambia hiyo ni
stoo wanawekaga mavitu yamejazana humo basi wakakiacha wakaondoka.
Hawakuishia hapo bado waliendelea kumsaka Hamida bila mafanikio.
Hamida alipotea toka jumapili iliyopita,jumanne juzi
kila mtu wakapanga kila mtu akamtafute popote pale anapoona anaweza
kumpata.Mama akaenda kwenye maombi kanisani wakati muislam,dada akaenda
blue pearl kazini kwa Yahaya
na huku majirani Mbagala wakaanza kuona inzi na harufu kali ikitoka
nyumbani kwa Yahaya.Ikabidi mjumbe apige simu kwa mama Hamida kumueleza
kinachoendelea polisi wakaitwa,nyumba ikavunjwa ili kutafuta harufu
inatokea wapi.Wakavunja kile chumba cha stoo na kukuta mwili wa Hamida
umeshaanza kuharibika.Kanyongwa na kamba ya katani na kitenge kafungwa
puani na mdomoni.Mwili wake ukawekwa kwenye mfuko akajaziwa mito na
manguo nguo na tendegu la kitanda kawekewa shingoni.
Ndugu, polisi wakachukuwa mwili kwa ajili ya msiba na mazishi wakati huo Yahaya alishakimbia siku nyingi hajulikani alipo.
Hamida alizikwa jana kule kwa babu yake Mzenga
uzaramuni walipokuwa waende kwenye mashamba waliyopewa. Msiba upo
nyumbani kwao Tabata. Mrehemu ameacha mtoto wa kike wa miaka mitatu
anaitwa Tayana.
Habari hii inaendelea tena kesho katika heka heka za leo ndani ya leo tena ya clouds fm.
R.I.P Hamida na tunatoa pole kwa familia nzima ya Urembo kwa msiba
poleni wafiwa, hasa mtoto! roho yauma haswa
ReplyDelete