Polisi mkoani Kilimanjaro, imemtia mbaroni daktari mstaafu wa Hospitali ya Serikali ya Mkoa ya Mawenzi kwa tuhuma za kumtoa mimba msichana wa miaka 17.
Tukio hilo linadaiwa kutokea juzi, ambapo Dk huyo
anayedaiwa kuwa na umri wa miaka 50 (jina tunalo), alikamatwa saa 10:45
alasiri katika nyumba ya mjomba wake iliyopo eneo la Kiboriloni mjini
hapa akiwa katika harakati za kufanya tukio hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz
aliwaambia wanahabari jana kuwa, uchunguzi umebaini msichana aliyekuwa
akitolewa mimba ni mhitimu wa Chuo cha Ualimu Masama Suni.
Kwa mujibu wa Kamanda Boaz, msichana huyo amelazwa
katika Hospitali ya Mawenzi akiendelea kupatiwa matibabu baada ya
jaribio hilo la kumtoa mimba kuzimwa na polisi kabla halijakamilika.
Katika tukio kama hilo, daktari mmoja aliwahi
kumsahau mwanafunzi aliyekuwa akimtoa mimba na kwenda kunywa pombe na
baadaye mwanafunzi huyo alipoteza maisha. Desemba 20,2012 Polisi
lilimtia mbaroni daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama pia.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....