Kijana Godfrey Masharo mkazi wa mjini Iringa akivuja damu baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali kifuani na watu wasiofahamika usiku wa jana wakati akitoka kujirusha disco
WATU wasiofahamika wamemvamia na kumchoma na kitu chenye ncha kali kifuani mkazi wa mjini Iringa Godfrey Masharo (pichani) .
Tukio hilo limetokea jana usiku majira ya saa 11 alfajiri wakati kijana huyo akitoka kujirusha katika kumbi za starehe mjini hapo.
Akizungumza kwa tabu na mtandao huu kijana huyo anadai kuwa watu hao watatu ambao hawafahamiki kwa majina walimvamia na kumchoma na kitu hicho chenye ncha kali kifuani na kukimbia .
Alisema kuwa tukio hilo limetokea eneo la Miyomboni barabara kuu ya Iringa -Dodoma jirani na jengo la Hazina Ndogo ya mkoa wa Iringa .
Umeona kifuani.....ni hatari sana
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....