Mwili wa mwalimu aliyeuwawa kwa kupigwa risasi na polisi Makete kisa kutovaa Helment (kofia ya pikipiki)
Akizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com mkuu wa polisi wilaya ya Makete SP Peter Kaiza kuhusu tukio hilo lililotokea eneo la benki ya NMB tawi la Makete jana majira ya saa moja na robo alisema kuwa mwalimu huyo alikuwa anakwenda kupata huduma za kibenki kupitia mashine ya kutolea pesa ya ATM akiwa na pikipiki ndipo alipo amuliwa na askari mmoja aitwae Jose Msukuma na kukutwa na umauti huo .
Inadaiwa kuwa kisa cha mauwaji yake ni madai kutovaa kofia hiyo na baada ya kuitwa na askari hao alikaidi amri na kutaka kumgonga askari huyo aliye kuwa lindo.
Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Idd Nganya ambaye ndie mwajiri wa marehemu amesema kuwa mwili wa marehemu bado umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya makete wakati utaratibu wakusafirisha mwili huo kwenda kwao mbeya kwa ajili ya mazishi ukiendelea
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye jina lake limehifadhiwa amesema kuwa askari hao walikuwa wakiomba fedha kwa mwalimu huyo na baada ya kukataliwa ndipo walipo anza kumshushia kichapo na alipo wazidi walilazimka kutumi asilaha na kumpiga begani kwa risasi
Walimu wenzake na marehemu ambao walifika hospitali kujua kuhusina na kifo cha mwalimu mwenzake wameeleza kusikitishwa na tukio hilo na kulifananisha na tukio la kikatili machoni pao
Mganga mkuu mfawidhi ambaye ni msemaji wa hospitali ya wilaya ya makete Dr Michael Gulaka amesema kuwa wao walipokea mwili wa marehemu na sio majeruhi
Chanzo: francisgodwin.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....