HOSPITALI YA RUFAA YA MOROGORO YASIKITISHA, WAUGUZI WASHIKILIA "DRIP" KWA KUKOSA MLINGOTI...!!

BAADHI ya wananchi wameshangaza na kitendo cha waunguzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kupokezana kuwashikia “infusion drips” maarufu kama ‘dripu’  ya chupa ya dawa wagonjwa waliolaza chini kwenye wodi za hospitali hiyo ya rufaa nya mkoa wa Morogoro baada ya kukosa vitanda.


Kadhia hii inainazidi kuiandama hospitali hiyo ambayo imepandishwa hadhi ya kuwa Hospitali ya Rufaa hivi karibuni ambapo ljumaa iliyopita mtangazaji wa Top Radio ya mkoani hapa Edward Abed Mganga aliyevamiwa na majambazi na kukimbizwa kwenye hospital hiyo, ameimeilalamikia hospitali hiyo kwa kumtelekeza bila kumpa huduma kwa zaidi ya masaa matano na kulazimika kuondoka kwenye hospitali hiyo ya serikali na kwenda kutibiwa hospitail za watu binafsi.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia waunguzi wa hospitali hiyo wakipokeza kuwashikia  dripu wagonwja.

Juzi hospitali hapo walijaa majeruhi zaidi ya 60 waliokuwa wamedhurika baada ya kiwanda  cha kutengeza nguo za michezo cha Mazava kukumbwa na hitilafu ya umeme wakiwamo ndani na hivyo kuwahishwa kwenye hospital hiyo na hivyo uongozi wa hospitali hiyo baada ya kuelemewa ulilazimika kutoa magodoro kutoka stoo na kuwalaza chini baadhi ya majeruhi hao kutokana na upungufu wa vitanda.

Bi Asha Abdallah aliyekuwepo ndani ya wodi namba 3 walipolazwa majeruhi hao alikuwa na haya ya kusema
Hii ni aibu kubwa kwa hospital ya rufaa ya mkoa kuwalaza chini wagonjwa hata kama wakijitetea kwamba wagonjwa wamekuja kwa mkupuo. Hospitali inapopewa hadhi ya Rufaa inamaana inamudu kukabiliana na majanga yoyote kwa maana wa kuhudumua majeruhi zaidi ya mia watakaofikisha kwa mkupuo kwenye hospitali hiyo.
Mwandishi wa habari hizi mbali ya kushuhudia wauguzi hao wakipokeza kuwashikia dripu wagonjwa, pia walishuhudia wahudumu hao wakilazimika kuwaruka juu wagonjwa waliolazwa kwenye eneo la njia za wodi hizo, jambo ambalo ni hatari sana.


Ili kupata ufafanuzi wa jambo hilo mwandishi wa habari hizi alimtafuta Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo kwa zaidi ya siku tano na kufanikiwa kumpata asubuhi  ya leo ambapo alipotakiwa kuzungumzia hali hiyo, Mganga huyo mfawidhi Dk Rita Lyamuya alikuwa na haya ya kusema:
Ni kweli siku ile ya tukio la kiwanda cha Mazava tulitoa magodolo stoo na kuwatandikia chini baadhi ya majeruhi. Kiukweli kwa issue kama ile tulikosa namna ya kukabiliana  nayo kwani walikuja kwa mkupuo zaidi ya majeruhi 65 hivyo tulichofanya tuliwapokea na baadhi kuwalaza chini na kuwapatia huduma ya kwanza huku kukitafuta sehemu muafaka ya kuwalaza.
  

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter