Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya nchini humo, kahaba huyo aliyejitambulisha kwa jina la Ester Mwende, awali alifuatwa na mtumishi huyo wa Mungu na kumtaka wafanye mapenzi zoezi ambalo lilifanyika.
Akasema baada ya zoezi hilo, ndipo mtumishi huyo wa Kanisa la Fire Ministries Embakasi alimtaka afike kanisani hapo ili kutoa ushuhuda wa uongo na kumuahidi kwamba angemlipa kiasi cha shilingi 10,000 za Kenya (kama 180, 000 za Tanzania).
Mwande ambaye alikuwa akitoa ushuhuda huo kwenye Kituo cha NTV cha nchini humo, alisema alikubali na kesho yake alikwenda kanisani kwa mchungaji huyo anayesifika sana kwa miujiza na upako.
Akasema: Nilipofika nilikaa na kujifanya nimepinda midomo. Muda wa maombezi mchungaji akasimama na kusema mimi nina matatizo, nimepinda midomo kwa sababu kuna kanisa nilikwenda nikasema kuna mchungaji amebaka mtu kwa hiyo pigo langu lilikuwa kupinduka midomo.
Mwande aliendelea kusema kwamba mpaka anatoka kanisani hapo bado alikuwa amejipindisha midomo jambo lililomfanya kila mtu aliyemuona aamini.
Akasema kesho yake alirudi tena na muda wa watu kushuhudia uponyaji, yeye alitoka mbele. Mchungaji alipomwona aliwaangalia watu na kuwaambia: Huyu mama ni yule aliyekuja jana akiwa amepinduka midomo kwa sababu ya kuwasema vibaya watumishi wa Mungu.
Mwande alisema alishuhudia kwamba baada ya maombezi ya siku iliyopita anamshukuru Mungu alimponya na midomo yake iko sawasawa kama zamani, kauli iliyosababisha kanisa zima kulipuka kwa shangwe za kumtukuza Mungu.
Mwande alisema aliamua kuweka wazi madai hayo baada ya mtumishi huyo kumrusha fedha nyingine walizokubaliana akidai kwamba mbali na yeye pia mchungaji huyo alimtaka amtafutie makahaba wengine watatu, jambo ambalo alilitekeleza lakini nao pia hakuwalipa.
Makahaba wenzake Mwande, wao walisema walimtumikia mtumishi huyo kwa kutoa shuhuda za uongo lakini hakuwalipa ujira wao na walipomfuata aliwajeruhi miguuni.
Walisema baada ya tukio hilo, walitoa ripoti kwenye Kituo cha Polisi cha Embakasi lakini maafande hao walikuwa wakisuasua kumtia mbaroni mtumishi huyo.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....