MREMBO wa Ruvuma mwaka 2006, Isabella Mpanda ‘Bella’, Jumamosi iliyopita alimshushia kipigo mpenzi wake ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Fleva, Kalama Bakari ‘Luteni Kalama’ baada ya kumnasa akipiga soga na mwanaume anayedaiwa kuwa shoga.
Kalama Bakari ‘Luteni Kalama’ (kulia) akizuia asiendelee kupewa kichapo na mpenzi wake, Isabella Mpanda ‘Bella’.
Sakata hilo lilitokea kwenye Baa ya Meeda, Sinza Mori, Dar ambapo Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ ilikuwa ikikamua.Kabla ya tukio, Kalama na Bella waliingia ukumbini hapo mishale ya saa saba usiku, Bella akiwa mbele huku akiongea akijua yupo na mpenzi wake, alipogeuka akajikuta akiwa peke yake.
Kitendo hicho kilimfanya mrembo hiyo avue viatu na kumrudia Kalama.
“Yaani wewe ni wa kunidhalilisha mimi? Unafikia hatua ya kutembea na mashoga siyo? Leo utanieleza mlitaka kufanya nini?” alisikika Bella huku akimrushia ngumi jamaa yake.
Hata hivyo, dhoruba hiyo ilitulizwa na maninja wa baa hiyo wanaofanya kazi ya kuhakikisha usalama wa wateja.
“Anataka kuniletea za kuleta, mimi siwezi kumvumilia, ananisaliti mimi?! Yule mwanaume ni shoga tu nani asiyejua na Kalama namjua bwana,” alisema Bella alipoulizwa na paparazi wetu.
Kalama: “Jamani mimi namshangaa sana Bella, ndiyo ni demu wangu lakini da! Sasa too much. Yule jamaa namfahamu, nilikuwa namsalimia tu, yeye kapaniki kama nini, huku ni kutiana aibu bwana.”
Kama vile hilo halitoshi, Jumatatu iliyopita katika Hoteli ya Villa, jijini Dar wawili hao walizua tafrani nzito baada ya kutwangana ndani ya chumba usiku mnene.
Chanzo kilisema kuwa, wawili hao walichukua chumba kwenye hoteli hiyo kwa ajili ya kupumzika na ‘mastresi’ yao, lakini muda mfupi baadaye walianza kuzozana huku Kalama akimpa Bella ambaye alipiga kelele kuomba msaada.
Mlinzi wa hoteli hiyo aliposikia kelele za Bella alikwenda na kuamuru mlango ufunguliwe na ndipo mrembo huyo akapata upenyo wa kukimbia.
Bella akiondoka kwa hasira baada ya timbwili hilo.
Hata hivyo, habari zinasema kutokana na varangati lililotokea, Kalama hakuruhusiwa kulala hotelini hapo, hivyo alianza safari ya kurudi nyumbani kwake, Tabata, Dar.Akiwa maeneo ya Buguruni, usiku huo, Kalama alikamatwa na polisi waliokuwa doria wakimdhania ni kibaka na kufikishwa katika Kituo cha Polisi Sitakishari na kulala hapo mpaka asubuhi alipokwenda kutolewa na marafiki zake.
Alipotafutwa Kalama kuelezea hali hiyo, alisema: “Naona pombe ndizo zilisababisha nimpige Isabella lakini nimemuomba msamaha hataki, nampenda sana huyu mtoto.”
Alhamisi Risasi Jumamosi lilimsaka Bella kwa simu na kumuuliza kuhusu ishu hiyo akasema:
“Yaani mapenzi yananishinda kwa sababu kila siku Kalama ananipiga lakini alivyonipiga safari hii ni zaidi ya siku zote, kama siyo mlinzi ningekufa, kosa langu kumwambia ukweli kwamba rafiki yake (hakumtaja jina) ananitongoza,” alisema Bellah.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....