Yaani imekuwa ni kitu cha kawaida sana kwa wanachi hususani wakazi wa vijijini kujisaidia PORINI!! Hali hii ya uchafuzi wa mazingira haivumiliki kwa namna yoyote ile kwani hakuna sababu maalum kwa mtu yeyote kutenda jambo kubwa la uchafuzi wa mazingira.
Wanaoonekana kwenye picha hiyo hapo juu ni wanachi wa kijiji kimoja mkoani MOROGORO ambao walinaswa na CAMERA yetu wakisaidia kando kidogo ya barabara ielekeayo DODOMA.
Kitu cha kushangaza zaidi tabia hii imeonekana kuwa ni utamaduni miongoni mwa wananchi ambao wengi wao wamekuwa wakifanya hivi pengine kwa kutokujua madhara yatokanayo na uchafuzi huo wa mazingira ikiwemo ni pamoja na mlipuko wa magonjwa mbali mbali kama vile kuhara damu pamoja na kipindupindu.
Wananchi mnaaswa kuzingatia kanuni za usafi jamni kwani kutunza mazingira ni jukumu letu wote,
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....