DAVINA, SANDRA SASA NI BIFU ZITO!!

MASTAA wa filamu wenye majina makubwa Bongo, Halima Yahya ‘Davina’ na Salma Salmin ‘Sandra’ wapo ndani ya bifu zito baada ya Davina kudaiwa kumtupia tuhuma mwenzake huyo kuwa ana mpango wa kumrudisha katika umaskini baada ya kuukata kimaisha.




 
Halima Yahya ‘Davina’.
Kwa mujibu wa chanzo, maendeleo ya Davina ni gari moja aina ya Toyota IST na kupangishiwa nyumba, Mbezi, Dar na mwanaume mmoja (jina tunalo) ambaye uhusiano wao uliunganishwa na Sandra.
Sosi alisema kuwa haijulikani kwa nini Davina ameamua kumchukia Sandra na kumshushia madai hayo wakati anahusika kwa asilimia mia moja kumuweka mahali pazuri.
Cha kushangaza, chanzo kikasema, Davina hataki suluhu akidai hawezi kuwekwa chini na hasimu wake huyo japokuwa Sandra aliitikia wito wa kikao.
Paparazi wetu siku ya Jumanne alimvutia ‘waya’ Davina na kumsomea mashitaka yake, akasema kwanza yeye ni mtu mzima hajawahi kukuwadiwa bwana tangu azaliwe na haitotokea, kisha akakiri kutokuwa karibu na Sandra kama zamani. Alipoulizwa sababu alikata simu.
Salma Salmin ‘Sandra’.
Maswali yalihamia kwa Sandra ambaye alifunguka: “Unajua mwandishi namshangaa Davina! Sikutarajia angenifanyia hivyo wakati mimi ndiye
nimemuweka kwa mtu mwenye fedha na kupata maendeleo aliyonayo sasa, siwezi kukwambia mimi na yeye tuna bifu gani.
“Yeye baada ya kumpata kaka yangu akaanza kumwambia maneno ya kumfanya anichukie akijua labda nitamwambia mambo yake ya siri, niliposikia nikamuita nimuulize akaniambia yuko bize na mwanaume wake, visingizio kibao.”
“Mimi nikitaka kumharibia Davina ni mara moja tu, kwanza mwanaume huyo hakumpenda yeye alimpenda Lissa (hakutaja jina la pili) lakini mimi niliona kwa sababu yeye namjua zaidi ndiyo nikamuweka hapo. Sasa kapata ananiona wa nini.”  

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter