SITUMII MWILI WANGU KUIBA WANAUME WA WATU,NATOA PENZI KWA MTU NIMPENDAYE- Agness Masogange



MWANADADA anayejipatia umaarufu kupitia video za wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Agness Masogange, ameuambia mtandao Huu kuwa hatumii mwili wake kama chombo cha kuwakamata wanaume bali hutoa penzi lake kwa yule anayempenda na ishu zinazozungumzwa mitaani kuwa anaongoza kwa kuiba wanaume za watu si kweli na wanaodai hivyo hawamtakii mema.

Mwandishi wetu alizungumza na mwanadada huyo juu ya ishu kadhaa zinazongumzwa juu yake, ndipo alipofunguka kuwa hatumia uzuri wake au umbo lake kama njia ya kuwavuta wanaume kwani angeamua kufanya hivyo basi angekuwa na wanaume wengi sana.

“Mwili wangu si chombo cha kuwakamata wanaume na hao watu wanaosema kuwa naongoza kwa kutembea na wanaume za watu ni wale wenye nia ya kunichafua kwani mi si demu wa hivyo,” alidai.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter